SERIS FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA VIJANA WAHANDISI JUU YA UJASIRIAMALI NA UBUNIFU
TAASISI ya SERIS (Seris Foundation) yenye makao makuu yake Ilala, Jijini Dar es Salaam leo oktoba 23, 2024 imefungua rasmi mafunzo ya vijana wahandisi juu ya ujasiriamali na ubunifu.Mafunzo yamefunguliwa rasmi na Msajili msaidizi wa Jiji la Ilala kuleta salam kutoka Serikalini Bi. Mwanaisha Boffu ambapo alikuja kuwakaribisha rasmi vijana katika mafunzo haya na kuwaelezea fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na Serikali.Kwa upande wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) Bi. Rose Isack Shayo ambaye alikuja kumwakilisha Msajili wa ERB alileta salamu kutoka Kwa msajili na kuwaelezaa vijana wahandisi namna ambavyo bodi inakuwa fursa mbalimbali kwa wale ambao wamesajiliwa, na kusisitiza kuwa hata mafunzo haya ambayo yametolewa na Seris Foundation ni matokeo ya wao kusajiliwa na ERB. Nae CPA. Deborah Wami ambe ni CEO wa Seris Foundation katika ufunguzo huo aliwakaribisha katika Mafunzo vijana Maenjinia na kuwataka kutumia mafunzo hayo kama fursa ya wao kuanzisha vikundi ambavyo vitawapeleka katika hatua nyingine wa kuanzisha miradi yao binafsi na kuacha na dhana ya kuajiriwa. Mafunzo haya yameanza leo katika chuo cha Technolojia cha Dar es Salaam (DIT) na yatamalizika siku ya Jumamosi.