SIKU YA PILI YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA UBUNIFU KWA WAHANDISI VIJANA
Siku ya pili ya mafunzo ya kitaalamu ya Ujasiriamali na Ubunifu ambapo zaidi ya wahandisi vijana 100 walihudhuria. Katika picha ni Bi. Neema Bawairu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) akiwasilisha kuhusu fursa za udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili zinazotolewa na EU. Pia, Mkurugenzi Mtendaji wa SERIS Foundation CPA Deborah Wami akiwasisitiza wahandisi vijana kuomba udhamini huu kwani una manufaa mengi.Picha ya mwisho ni Seris Foundation Members na European Union mara baada ya kufanya mawasilisho ya fursa zinazotolewa na Umoja wa Ulaya katika Masomo ya Shahada ya juu. Mafunzo haya yanaendelea mpaka siku ya Jumamosi tarehe 26 Oktoba , 2024 katika chuo cha DIT.